Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga niqab kichwani.
Jamaa za mwanamke huyo mwenyeji wa mji wa
Hosingow kusini mwa Somalia wanasema mwanamke huyo alikataa kujifunika
kitambaa kichwani kuambatana na sheria za dini ya kislamu .
''alikuwa
ameonywa ajisitiri lakini wapiganaji hao waliporejea wakashikwa na
hasira walipopata kuwa hakuwa amejifunika na hivyo wakampiga risasi''.
Jamaa zake wameiambia BBC kuwa Ruqiya Farah
Yarow alikuwa amewafokea wapiganaji hao akiwataka waondoke kwake na
kusema kuwa angejisitiri baadaye.
Kundi la Al Shabab linalomiliki asili mia kubwa
ya maeneo ya Kusini na Katikati ya Somalia na limekuwa likishinikiza
kutumiwa kwa sheria kali za kiislamu.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo amekanusha kuwa ni wao waliomuua mwanamke huyo .
Msemaji huyo anasema kuwa licha ya kudhibiti
maeneo makubwa nchini humo kundi hilo bado halijatoa maelezo ya vipi
wanawake wanastahili kujisitiri.BBC
No comments:
Post a Comment