Moja ya ajali ya magari ya abiria
Watu 17 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Dodoma.
Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya magari mawili, moja lori na jingine basi la abiria kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma David Misime
amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili za asubuhi siku ya leo imesababishwa na kile kinachodaiwa kuwa uzembe wa dereva la
gari moja lililohusika katika ajili hiyo.
Amesema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na
Lori ambayo yaligongana uso kwa uso baada ya dereva wa lori kujaribu
kulipita gari jingine bila kuangalia vizuri na hivyo kujikuta
yakigongana.
Tayari polisi wa Tanzania wameanza uchunguzi ili
kujua chanzo cha ajili hiyo lakini hata hivyo imeshindwa katika hatua
za awali kumshikilia mtu yoyote kwa vile maderava na magari yote ni
miongoni mwa walikufa katika ajali.
Hii si mara ya kwanza kwa ajali kama hii kutokea
hapa Tanzania ambapo sababu kadhaa zimekuwa zikitajwa kusababisha
ikiwemo mwendo kasi wa magari, uzembe wa madereva, pamoja na ubovu wa
barabara.
No comments:
Post a Comment