Bodi ya usajili
ya wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi(AQSRB)imesema utumiaji wa teknolojia
ya kisasa katika sekta ya ujenzi ni jibu la uhakika la changamoto nyingi
zinazoikabili sekta ya maendeleo ya miundombinu Tanzania.
Rais Obama
yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na
shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukrain. Kwenye hotuba muhimu
kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama wa Marekani na
nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.
Popo
hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi ya maeneo ya Guinea,
lakini sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola
kusini mwa nchi hiyo. Maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na
ulaji wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola,
ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
No comments:
Post a Comment