Pages

Thursday, May 22, 2014

WIMBO WA PHARRELL "HAPPY" WAZUA ZOGO IRAN

Kikundi cha mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga wimbo maarufu wa mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams, 'Happy' wamejipata matatni baada ya kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.


Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.

Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa Iran wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita wakisherehekea na kujiburudisha kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya kukiuka maadili.

Hata hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.

"waliniambia kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana nikakubali kushiriki,'' alisema mmoja wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.

                                          Kanda hiyo imetazamwa na watu 40,000
'Wamekiuka maadili'
Kulingana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13 walikamatwa kuhusiana na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa haijatangazwa rasmi.

Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu ambao umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea kukasirishwa na hatua ya vijana hao kukamatwa.
"yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,'' alisema Pharrell katika ukurasa wake wa Facebook.
                                         Pharrell aliteuliwa kwa tuzo la Oscar mwaka huu

Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.

Kanda hiyo ya "Happy we are from Tehran" ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.

Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy' umepelekea maelfu ya watu kote duniani kuiga video ya wimbo huo na kutengeza video zao wenyewe. Kutoka Kenya, Marekani , Uingereza yaani nchi nyingi duniani tu, watu wameiga video hiyo kwa kutengeza yao wenyewe.BBC

No comments:

Post a Comment