Pages

Thursday, May 22, 2014

APATIKANA MIAKA 10 BAADA YA KUTEKWA NYARA

                                                 Amevumilia unyanyasaji kwa miaka kumi

Mwanamke mmoja, wa miaka 25, aliyepotea miaka 10 iliyopita, amewaambia polisi kuwa alilazimika kuolewa na aliyemteka nyara na kisha kupata mtoto naye.
Mwanamke huyo, kutoka Santa Ana, ambaye jina lake halikutajwa, aliwasiliana na polisi baada ya kumpata dadake katika mtandao wa Facebook.


Isidro Garcia, mwenye umri wa miaka 41, alikamatwa Jumanne kwa tuhuma za kuteka nyara, kubaka na kumdhulumu mwanamke huyo.
Katika taarifa yao, polisi walisema kuwa Garcia alikua anaishi na familia ya mwanamke huyo wakati ambapo alitoweka.

Unyanyasaji wa miaka kumi
Taarifa hiyo ilisema kuwa unyanyasaji huo ulianza mwaka wa 2004, wakati ambapo Garcia na mamake muathiriwa walikua wachumba.
Garcia aliishi pamoja na mamake muathiriwa na wanawe wa kike huko Santa Ana, ambao ni mji katika kaunti ya Orange.

                              Garcia alimteka mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 15

 Madai ya polisi ni kuwa Garcia alianza kumnyanyasa kijinsia mwathiriwa katika mwezi wa Juni, mwaka huo.
Miezi miwili baadaye, alimshambulia mamake muathiriwa, kisha akamleweshaa msichana huyo, na kumpeleka maili 26 kaskazini, hadi Compton, alikomfungia na kumzuia.

Garcia alimtisha msichana huyo dhidi ya kurudi kwa familia yake.
Wawili hao waliikwepa polisi kwa muda
Mara nyingi, Garcia alimdhulumu msichana huyo kimwili na kwa njia ya ngono.

Maisha ya kifungo
Walifanya kazi pamoja katika huduma moja ya usafi, usiku. Muathiriwa alishindwa kabisa kujinusuru na aliendelea kuishi na Garcia akidhulumiwa.
Mwaka wa 2007, Garcia alimlazimisha mwanamke huyo waoane na mwaka wa 2012, wawili hao wakapata mwana.

Ni juzi tu, ambapo muathiriwa huyo aliwasiliana na dadake kupitia mtandao wa Facebook na hatimaye alipata ujasiri wa kuwasiliana na polisi.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa polisi waliitwa katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu jioni ili kuhudumia tukio la kinyumbani na ndipo muathiriwa huyo akawaambia alikua ametekwa kwa muda wa miaka 10.
Garcia aliyekamatwa Jumanne, bado hajasomewa mashtaka yake kamili.BBC

No comments:

Post a Comment