Jeshi linaendelea kuwasaka wapiganaji Boko Haram
Wasichana waliotekwa nyara na kundi lenye itikadi
kali za kidini, Boko Haram nchini Nigeria, wameielezea
BBC ukatili walio
upitia mikononi mwa kundi hilo.
Wakati wakizuiwa, wasichana hao walishuhudia watu kadhaa wakiwemo baadhi wanaotoka kijiji kimoja na wapiganaji wa kundi hilo, wakikatwa shingo.
Hili limefanyika miezi kadhaa iliyopita katika kambi moja katika eneo la mashambani, la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wakati huo huo msichana mwingine alieleza jinsi wapiganaji hao walivyo mlazimisha kumuua mwenziwe ambaye pia alitekwa nyara.
Wote walifanikiwa kutoweka kutoka kambi hizo na sasa wanaishi mafichoni.
Jeshi la Nigeria linasema linaendelea kuwasaka wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika eneo hilo lililo mashinani.
Wapiganaji hao wanaendelea kuyashambulia miji na vijiji katika kiwango cha kushtusha ambapo zaidi ya raia mia tano wameuawa katika wiki za kwanza za mwaka huu.BBC
No comments:
Post a Comment