Pamoja na mpango wa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuliaga Bunge kukwama jana, Chama cha
ACT- Tanzania kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kumpokea mwanasiasa huyo
kuanzia leo.
Serikali imeombwa
kuingilia kati mgogoro unaoendelea baina yake na nchi jirani ya Kenya, kuhusu
kuzuiliwa kwa magari ya Tanzania ya kusafirisha watalii kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Jomo Kenyata ili kuleta usawa na ustawi wa sekta ya utalii kwa
nchi zote mbili.
Rais Obama ametoa
ujumbe katika kanda ya video kwa viongozi na raia wa Iran akisema kwamba
hapajakuwa na wakati muafaka zaidi katika miongo kadha iliyopita kwa Marekani
na Iran kutafuta uhusiano mpya.
Uingereza imesema
itasaidiana na Kenya katika kukabiliana na makundi ya kigaidi ili kuboresha
amani kama njia bora ya kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo
mawili.Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amesema hayo baada
ya Kenya na Uingereza kutia saini mkataba wa maelewano baina ya mashirika ya
biashara na viwanda vya nchi hizo mbili.
Rais Obama amemtumia
salaam za pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutokana na ushindi
uliokipata chama chake katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.Lakini Bwana Obama
ameelezea dhamira yake ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na
Wapalestina kuwa ni kuunda taifa la Palestina.
No comments:
Post a Comment