Msanii wa kike anaetamba mwaka
huu na wimbo wa “Hellow Hellow Tanzania”
Linah Sanga amesema kazi anayoifanya haijawahi kufurahiwa na wazazi wake.
Linah aliyeibuka katika chuo cha
Muziki Tanzania House of Talent (THT),alisema kwa zaidi ya miaka sita sasa
anafanya kazi ambayo anaamini ipo siku atageuka kutokana na dhamira yake ya
kutaka kuwaridhisha wazazi wake.
“Ninachokiona ni kama
nimeasi,kutokana na kutosikiliza ushauri wa wazazi wangu walionileta
Duniani.Mashabiki wao wananihitaji na mimi pia ninatengeneza maisha.Naamini ipo
siku nitarudi kundini kwani wazazi hawafurahii muziki wa kidunia”alisema Linah
ambaye alikuwa akiimba nyimbo za Injili .
No comments:
Post a Comment