Serikali imetoa tamko kwa
madereva wa bodaboda kuwa hawaruhusiwi kufika mjini,na kama wanataka kufika
mjini basi inabidi wakate vibari vya City.
Wamiliki wa pikipiki hasa Makampuni
wanasema inakuwaje wakate vibali vingine wakati vile vya mwanzo bado
havijaisha,na kibari cha pikipiki moja ni sh 180,000.
Nimepata kuzungumza na moja ya
kampuni inayoitwa MOKA inayofanya
kazi za Clearing wao wanamiliki pikipiki
10 wao pia wanalalamika sana juu ya hili,sasa mfano wao wanamiliki pikipiki 10 ukipiga
hesabu 180,000 mara 10 jibu unapata ni sh Mil. 1,800,000.
Mmoja wa madereva waliokamatwa wa Kampuni ya MOKA ambaye hakutaka jina lake liandikwe anasema “Sasa
Serikali inakuwaje washindwe hata kuangalia swala hili kwa mapana,Inamaana wanataka
tulipie tena pesa na je hizo pesa tulizokatia vibari mwanzo ziko wapi?”
anaendelea kuongeza kwa kusema kuwa “Serikali inatuibia huku tunaona sasa
hatuelewi mtetezi wetu ni nani kama Serikali yenyewe ndo hii inakuwaje?”
Sijui wewe mtanzania unalionaje
swala hili ambalo linazidi kuvuta hisia za watu wengi,Kwamba hata kama ulikata
kibari kwa shilingi 180,000 unatakiwa kukata tena sasa je swali linakuja vipi
kuhusu peza za zilizokatwa mwanzo?
No comments:
Post a Comment