Pages

Thursday, April 03, 2014

DAVIDO AGEUKIA FILAMU



                                                                               Davido

Mkali wa miondoko ya Skelewu  Davido ataonekana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ambayo mpaka sasa haijapewa jina .Kwa mujibu wa tovuti ya Nigeriafilms,mwanamziki huyo anafanya kazi  chini ya muaandaaji mkongwe wa filamu,Teco Benson akishirikiana na binamu yake Kechukwu Ojeogwu ambaye ni mwigizaji.

“Ndiyo mara yake ya kwanza kuigiza,hivyo mwandaaji atampavipande vya kawaida ili kupata uzoefu ,vilevile aweru kuviigiza na kuweka mbwembwe “alisema Ojeogwu.

Hivi karibuni Davido akiwa katika ziara ya kimuziki nchini Marekani,alilazimika kukatiza shoo yake,baada mashabiki kuvamia jukwaani hali ambayo iliwalazimu polisi kuingilia kati na kusitisha onyesho hilo.

No comments:

Post a Comment