Kundi maarufu la muziki wa kwaito la nchini Afrika
Kusini,Mafikizolo linatarajia kutua
kesho jijini Dar es salaam kwa ajili ya onyesho litakalofanyika katika ukumbi
wa mlimani City April 5.Kundi hilo linaundwa na wasanii wawili Theo Kgosinkwe
na Nnlanla Nciza,litawasili nchini kesho mchana kwa ajili ya onyesho hilo.
Akizungumza na gazeti la mwananchi mratibu wa onyesho hilo
Vinny Magere kutoka kampuni ya Juegacassa,amesema mafikizolo wanatarajia
kufanya onesho moja tu maalumu litakalodumu kwa muda wa saa nne.
“Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kundi hili kufika
nchini,tangu kuachia wimbo wao “Khona “ Mashabiki wa burudani wanaujua wimbo
sana,ninaamini wana hamu ya kuwaona wenyewe wakiuimba moja kwa moja kutoka
jukwaani” alisema Vinny.
Mafikizolo kwa sasa wanashikilia taji la kundi bora la
mwaka,kwa mujibu wa Tuzo za muziki za
South Afican Music Awards (Sama)Katika kinyang’anyiro cha mwaka huu kwenye tuzo
hizo zenye vipengele 28,kundi hilo linawania katika vipengele vine tofauti
ambavyo ni :Kolabo bora ya mwaka ,Albamu bora ya mwaka na kundi bora la
mwaka.kundi hilo maarufu limewahi kutamba miaka ya nyuma na nyimbo kama “Ndihamba
Nawe,””Ndixolele”,”Sebeneza”,”Ndashata” na “Ndizolila”.
Kundi hili lilianza shuguli za muziki mwaka 1996 na
kufanikiwa kutoa albamu sita mpaka sasa.Miaka mitano nyuma kundi lilianza
kuteremka baada ya kila mmoja kutoa albamu yake binafsi.Mwaka jana waliungana
tena na kutoa albamu ya sita iliyoitwa “Reunited” na kutoa wimbo wao wa kwanza
“Khona“ ambao umewatambuisha upya na kuwarudisha kwenye chati.
No comments:
Post a Comment