WATOTO WA VIONGOZI NA SIASA
Nidhahiri kabisa kuwawatanzania wengi hawaridhiki na
mwenendo mzima wa sasa katika duru za siasa.Ni mwenendo wa kile kinachosemekana
kwamba ni mkakati wa makusudi wa viongozi wa siasa kuwarithisha watoto
wao,ndugu,au jamaa nafasi za uongozi
Kwa mfano mwaka 2012 chama hicho kilimpitisha Sioi Sumari
kugombea kiti cha Ubunge wa Arumeru Mashariki kilichoachwa na baba yake
Jeremiah Sumari alifariki dunia.Hata hivyo kijiti kilichoachwa na baba yake
kilimponyoka na kuchukuliwa na mgombea
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Joshua Nassari.
Sioi Sumari
Rais Jakaya Kikwete.
Ukimtoa Ridhiwani,Mkewe mama Salma Kikwete ni mjumbe
waHalmashauri kuu ya CCM.
Salma Kikwete
Ridhiwani Kikwete
Alhaji Hassan Mwinyi
Mtoto wake Hussein Mwinyi ni Mbunge na Waziri waulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.
Edwin Mtei
Chama alichokiasisi cha Chadema kinaongozwa na mkwewe ambaye
ni Freeman Mbowe.
Freeman Mbowe
Philemon Ndesamburo
Mwanae Lucy Owenya ni Mbunge wa viti maalumu wa
Chadema,Ambacho Ndesamburo no kada maarufu.Ndesamburo pia anamkwewe (mke wa mwanaye)Ambaye
ni Grace Kiwelu,Huyu ni mbunge wa viti maalumu Chadema.
Grace Kiwelu
Dk Wilbroad Slaa
Aliyewahi kuwa mke wake,Rose Kamilli ni mbunge wa viti
maalumu Chadema.Dk Slaa ni katibu mkuu wa Chadema .M chumba wake Josephine
Mushumbusi pia amekuwa akijishugulisha na siasa za chama cha mumewe.
Rose Kamili
James Mbatia
Ana dada aitwaye Nderakindo Kessy ambaye ni mbunge wa Bunge
la Afrika Mashariki nafasi aliyoipata kupitia NCCR-MAGEUZI.
Nderakindo Kessy
Yusuph Makamba
Mwanaye January Makamba ni Mbunge wa Bumbuli na
Naibu Waziri wa sayansi na Teknolojia.Makamba
aliwahu kuwa katibu Mkuu wa
CCM.Awali alishika
nafasi mbalimbali serikaliniJanuary Makamba
No comments:
Post a Comment