Pages

Thursday, March 20, 2014

CHRIS BROWN KUOGA MARA MOJA


Chris Brown anadaiwa kuwa ataruhusiwa kuoga mara moja tu ndani ya siku mbili akiwa jela. Staa huyo wa R&B alitupwa jela wiki hii ambako atakaa kwa mwezi mzima baada ya kufukuzwa rehab.

Brown atakuwa amefungiwa kwenye chumba chake mwenyewe kwa saa 23 kila siku, kwa mujibu wa TMZ. Hata hivyo ataweza kusoma vitabu na kufanya mazoezi na atakuwemo humo hadi tarehe 23 April.

Brown, 24 alifukuzwa rehab baada ya kumsogelea na kumshika mwanamke kinyume na masharti ya humo, kukataa kuchukua vipimo vya madawa ya kulevya na kwa kutoa kauli za vitisho wakati wa therapy ya kundi kwa kudaiwa kusema “I am good at using guns and knives.” UDAKU

No comments:

Post a Comment