Utafiti uliofanywa na shirika moja la misaada
Uingereza umeonyesha kuwa ubakaji unatumiwa tena kwa kiasi kikubwa
gerezani kama adhabu kwa wanawake wanaojihusisha na masuala ya siasa
nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Utafiti huo uliofanywa na "Freedom from Torture"
umegundua kuwa zaidi ya nusu ya wanawake wote walio fanyiwa uchunguzi
walikuwa wamebakwa na magenge.
Shirika hilo ambalo huwasaidia waathiriwa wa ubakaji umewafanyia
uchunguzi wanawake 34. Ubakaji umekuwa ukitumika kwa miaka mingi kama
silaha katika vita vya mashariki mwa DRC lakini shirika la
''Freedom
from Torture'' linasema kuwa sasa wanawake magerezani kote nchini humo
wanabakwa kama njia moja ya kuwaadhibu na kuwanyamazisha kutozungumza au
kuchangia siasa za nchi hiyo.
Wanawake hao waliofanyiwa uchunguzi wanajumuisha
wachuuzi, wasomi na hata wataalamu mbali mbali kati ya miaka 18 na 62
kote nchini humo.
Takriban hao wote walitiwa nguvuni kwa
kujihusisha na masuala ya haki za binadamu au kampeini za kisiasa, au
hata jamaa katika familia yao alihusika na siasa.BBC
Zaidi ya nusu ya wanawake hao wanasema wamebakwa
na magenge hata wanaofika kumi. Shirika hilo sasa linataka serikali ya
DRC kufanya hima kutekeleza azimio la umoja wa mataifa dhidi ya kuwatesa
watu.
No comments:
Post a Comment