Pages

Monday, June 02, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB),  Freeman Mbowe amemtunishia misuli, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema hawatishwi na kusudio alilotoa la kubadili kanuni ili kudhibiti tabia ya kambi hiyo kususia vikao vya Bunge kila wanapopinga hoja.

Polisi kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa shambulizi la bomu limewauwa zaidi ya watu 14 na kuwajeruhi wengine wengi.Ripoti zimesema kuwa mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mubi, ulilenga chumba kimoja cha burudani ambako watu walikuwa wakitazama mechi ya soka kwenye televisheni.

Utafiti uliofanywa na shirika moja la misaada Uingereza umeonesha kuwa ubakaji unatumiwa tena kwa kiasi kikubwa gerezani kama adhabu kwa wanawake wanaojihusisha na masuala ya siasa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Serikali ya Afghanistan imeghadhabishwa na makubaliano ya Marekani kukubali kuwaachia huru wanamgambo watano wakuu wa Taliban, ili kuachiwa huru kwa mwanajeshi wa Marekani.Wafungwa hao kutoka gereza la Guantanamo walikabidhiwa Qatar.

No comments:

Post a Comment