Pages

Tuesday, October 21, 2014

HABARI KWA UFUPI




Mwenyekiti  wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, amekunjua upya makucha yake yaliyowahi kurarua viongozi wenzake akiwa katika NCCR-Mageuzi na TLP, na sasa amefukuza hadharani madiwani wawili wa chama chake waliounga mkono nia ya Mbunge wa NCCR-Mageuzi, 


James Mbatia, ambaye ametangaza kugombea ubunge wa Vunjo.
Wakati Serikali ikiwekeza katika kupambana na ujangili nchini, imebainika kuwa raia kutoka China wamekuwa wakifanya ufisadi katika rasilimali za misitu hali inayohatarisha uhai wa rasilimali hiyo.

Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha limemuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa wa ugaidi, Yahaya Hassan Omari Hela (31) ‘Yahaya Sensei’ mkazi wa Mianzini mjini hapa.Mtuhumiwa huyo alipigwa risasi ya mguu na kalio la kulia eneo ya Kisongo wilayani Monduli alijaribu kuruka kwenye gari la polisi kwa lengo la kuwatoroka.

Ugonjwa wa Ebola unahitaji hatua za haraka na umakini katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, hii ina maana kuwa hatua hiyo inaondokana na taratibu za kawaida zilizozoeleka za mazishi katika nchi zilizoathirika, ikiwemo matumizi ya mifuko mikubwa ya plastiki ambayo ni mbadala wa majeneza.

Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema zaidi ya watu ishirini wameuawa katika mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa kundi la Boko Haram, licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufanyika ijumaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment