Pages

Friday, July 04, 2014

MGABE AWAFUKUZA WAKULIMA WAZUNGU

 Wakosoaji wa Mugabe wanasema sera ya mageuzi ya mashamba ilimalizika miaka miwili iliyopita

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.


"hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke,'' Mugabe aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.

Chama cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe yanasikitisha sana na kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.

Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 200-2009

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90, ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1980.
Alichaguliwa tena mwaka jana kwa asilimia 61 ya kura, na kumshinda mpinzani wake wa jadi Morgan Tsvangirai.

Chama cha Mugabe pia kilishinda viti vingi vya bunge na kupata 160 kati ya viti 210.
Mdadisi wa kisiasa nchini humo Stanley Kwenda anasema kuwa matamshi ya Mugabe, yanashangaza sana kwani serikali ilimaliza mageuzi ya sera ya umiliki wa mashamba miaka miwili iliyopita.

Inaonekana kwamba Mugabe anataka kuhujumu hali mbaya ua kiuchumi nchini humo kwa kuzungumzia maswala mengine ambayo hayana umuhimu kwa sasa.
Wananchi wa Zimbabwe wanakumbwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kufungwa kwa makampuni .
'Wasiwasi'

Mkulima huyu mzungu Zimbabwe,anatizama uharibifu uliofanyiwa nyumba yake baada ya watu kuivamia

"usiwe mkarimu sana kwa wakulima wazungu. Mashamba ni yako sio yao,'' alisema Mugabe alipotembelea mkoa wa Mashonaland , Magharibi mwa nchi.

Mtamshi ya Rais Mugabe, yalisababisha wasiwasi miongoni mwa wakulima wazungu. Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa wakulima wazungu Hendricks Olivier.

Ni wakulima 100 hadi 150 wazungu waliosalia nchini Zimbabwe, alisema Hendricks.
Maelfu ya wakulima walilazimika kuyaacha mashamba yao na kurejea walikotoka baada ya serikali kufanya mageuzi ya sera ya umiliki wa ardhi miaka 15 iliyopita.BBC

No comments:

Post a Comment