Siku mbili baada ya Kaimu Balozi wa Libya, Ismail Nwairat
kujiua kwa risasi akiwa ofisini kwake, Jeshi la Polisi kupitia kikosi maalum
cha uchunguzi wa matukio ya kujiua, limeanza uchunguzi wa kifo hicho.
Watu wasiofahamika wamemuua mkazi wa Kijiji cha Vikonge
Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Kitola Jeremia (45) kwa kumkatwa mapanga
sehemu za mwili wake sambamba na kumtoboa tumbo .
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu
waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.Chama
cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe yanasikitisha sana na
kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.
Mwanamke
mmoja aliyemtelekeza mwanawe ndani ya karatasi ya plastiki katika bustani moja
nchini Uingereza aponea adhabu ya kifungo jela.Mtoto huyo mchanga aliyekuwa wa
siku moja tu, alipatwa na mtu aliyekuwa anamtembeza Mbwa wake katika bustani
hilo.
Polisi
nchini Uganda wamedhibiti usalama mjini Kampala kufuatia onyo la mashambulizi
ya kigaidi kupangwa kufanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe.Maafisa
wa usalama katika uwanja huo, walisema kuwa onyo la shambulizi hilo
lililopangwa kufanyika Alhamisi linapaswa kuchukuliwa kwa uzito.
No comments:
Post a Comment