Daktari mmoja wa kuwatibu watoto katika hospitali ya
Cambridge nchini Uingereza amefunguliwa mashitaka kwa kosa la
kuwadhalilisha watoto wadogo kati ya umri wa miaka 11 na 15.
Daktari Myles Bradbury, mwenye umri wa miaka 41,
aliyefanya kazi ya kuwatibu watoto wadogo katika hospitali ya
Addenbrooke, anadaiwa kuwadhalilisha wagonjwa wake ambao walikuwa
watoto,kati ya mwaka 2011 na 2013.
Haijulikani ikiwa daktari huyo aliwadhalilisha watoto hao hospitalini au kwingineko.
Daktari huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Ijumaa.
Ameshitakiwa na makosa manne ya kuwadhalilisha watoto kingono na kuwachochea au kujihusiha kingono na watoto wavulana.
Pamoja na hayo anakabiliwa na kosa la kuwapiga watoto wadogo picha wakiwa uchi.
Daktari huyo tayari alifukuzwa kutoka katika hospitali hiyo.
Wazazi na watoto ambao wameathirika kutokana na vitendo vya daktari huyo wanapata ushauri nasaha.BBC
No comments:
Post a Comment