Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua maonyesho ya kimataifa ya utalii ya Swahili
Tourism Expo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba Mosi
hadi 4 mwaka huu.
Bodi
ya Mikopo ya Serikali za Mitaa nchini inatarajia kuanzisha Benki ya Maendeleo,
ili kuweza kukopesha halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi inayolenga kuchochea shughuli za maendeleo.
Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa
chama hicho kwa kuwa wanabanwa na katiba yao.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema jiografia ya
visiwa hivyo ni changamoto kubwa katika kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa
za kulevya.
Jeshi
la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa
Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini
humo.
No comments:
Post a Comment