Mwanamke akichunguzwa iwapo ana saratani ya matiti hospitalini.
Mazoezi yanaweza kusaidia kupona baada ya kuugua
saratani ya matiti lakini ni wanawake wachache sana wanashiriki katika
mazoiezi, utafiti unasema.
Watafiti wa Marekani, katika ripoti
waliyochapisha katika jarida linaloandika mambo ya saratani, wanasema
kuwa inajulikana wazi kwamba kufanya mazoezi ya aina moja au nyingine
kunasaidia lakini imegunduliwa kuwa wanawake hawapendi kufanya mambo
yanayowachosha.
Ni thuluthi moja pekee ya wanawake inayofanya mazoezi kufikia kiwango kinachopendekezwa.
Makundi ya kuwasaidia wanaougua saratani ya
matiti nchini Uingereza yanasema wanawake nchini humo wanahitaji
kusaidia wanawake kufanya mazoezi zaidi baada ya kutibiwa maradhi hayo.
Utafiti huo uliofanywa Marekani uliwashirikisha
wanawake 1,735 wenye umri kati ya miaka 20 na 74 waliokuwa na saratani
ya matiti kati ya mwaka 2008 na 2011 katika Carolina Kaskazini.
Marekani na Uingereza zinapendekezwa kuwa watu
wazima wanapaswa kufanya mazoezi ya kadiri ya dakika 150 kwa juma moja
au mazoezi makali zaidi ya dakika 75 kila wiki.
Lakini utafiti huu uligundua kuwa ni wanawake 35
pekee waliougua saratani ndio wanaofuata maagizo haya ya kufanya
mazoezi baada ya kutibiwa saratani ya matiti.
Nchini Uingereza wahamasishaji wa saratani ya matiti wanasema wanawake wanapaswa kufanya mazoezi mengi zaidi nchini humo.
Caroline Dalton, kutoka kundi la Breakthrough
Breast Cancer, alisema: " Mazoezi ya maungo baada ya mtu kuugua saratani
ya matoto yanaimarisha uwezekano wa aliyeugua saratani kupona kabisa na
kuna ushahidi pia kuwa yanasaidia kuhakikisha kuwa saratani ya matiti
haimrudii aliyeugua tena.
"Kuendelea na mazoezi pia kunasaidia mgonjwa
kustahimili, wakati wa matibabu na baadaye, kwa kuimarisha afya yake kwa
ujumla na kuisha maisha bora."
Aliongeza: "Ingawa utafiti huu ulifanyiwa
Marekani badala ya Uingereza, matokeo yanapendekeza kuwa wanawake ambao
wamegunduliwa kuwa na saratani ya matiti wanapaswa kusaidiwa ili
waendelee kufanya mazoezi."
"Hakuna mwelekezo kamili wakati huu kutueleza
kikamilifu kiwango cha mazoezi kinachohitajika baada ya kugunduliwa kuwa
una saratani ya matiti, lakini Breakthrough Cancer inapendekeza kuwa
unapaswa kulenga kufanya mazoezi kwa masaa matatu u nusu kwa wiki moja,
baada ya kushauriana na matabibu wako kukuelezea kiwango kinachokufaa."
Baroness Delyth Morgan, Afisa Mtendaji katika
Breast Cancer Campaign, alisema: "Utafiti huu unapaswa kuwakumbusha wote
kuwa ni muhimu kwa wanawake walio na saratani ya matiti kuwa kufanya
mazoezi kunachangia pakubwa kama wataishi au kufariki baada ya
kugunduliwa kuwa una saratani.
"Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa hata
nyongeza ndogo ya mazoezi yanayofanywa baada ya kugunduliwa kuwa mtu ana
saratani yanaongeza nafasi kwa mwanamke anayeugua kunusurika.
"Hii ndio sababu ni muhimu kwa wakawake kupewa
mpango kamili wa kufuata ulioandikwa chini ambao utasaidia ushauri
nasaha kuhusu maisha yao juu ya aina ya chakula na mazoezi."BBC
No comments:
Post a Comment