Pages

Monday, June 09, 2014

BRAZIL 2014:MAMBO 20 MUHUMU YA KIHISTORIA KATIKA KOMBE LA DUNIA

1 — Mechi zote za Kombe la Dunia 1930 nchini Uruguay  zilichezwa kwenye jiji moja: Montevideo.

2 — Beki wa Sweden, Jan Olsson, alikuwa akivaa jezi namba 2, beki huyo ndiye aliyemdhibiti vilivyo nyota wa Uholanzi, Johan Cruyff aliyekuwa akisifika kwa aina yake ya ugeukaji  na kuwatoroka mabeki “Cruyff Turn” kwenye fainali za mwaka 1974, Ujerumani Magharibi.

3 — Gwiji wa Brazil, Pele ni mchezaji pekee aliyetwaa  makombe matatu ya dunia akiwa anacheza mwaka: 1958, 1962 na 1970.


4 — Idadi ya wachezaji waliofunga mabao matatu katika mechi  mbili za Kombe la Dunia: Mhungary Sandor Kocsis (zote mwaka 1954), Mfaransa, Just Fontaine (1958), Mjerumani,  Gerd Muller (1970) na Gabriel Batistuta (moja 1994 na moja 1998).

                                                                        Just Fontaine
                                                                   Gerd Muller
                                                              Gabriel Batistuta

5 — Mshambuliaji wa Russia, Oleg Salenko ndiye  anayeshikilria rekodi ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya Kombe la Dunia, wakati Russia waliposhinda 6-1  dhidi ya Cameroon fainali za 1994 nchini Marekani.

                                                                       Oleg Selenko

6 — Paolo Rossi alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia  mwaka 1982 nchini Hispania, alipofunga mabao sita na kuongoza Italia kutwaa taji la tatu.

                                                                     Paolo Rossi

7 — Ni idadi ya siku ambazo Kombe la Dunia lilipotea baada ya kuibiwa mwaka 1966 nchini England. Mbwa aliyekuwa akiitwaa Pickles, aliyekuwa akitembea na mmiliki wake kusini mwa London, aliliona kombe hilo likiwa limefichwa kwa kuzungushiwa na magazeti kwenye kichakani wiki moja baada ya  kupotea kwake.

8 — Scotland ni nchi iliyofuzu mara nane kushiriki Kombe la Dunia. Lakini katika mara zote nane ilizoshiriki imeshindwa kufuzu kwa raundi ya kwanza.

9 — Ni rekodi ya Mexico ya kufungwa mechi tisa mfululizo za  fainali za Kombe la Dunia (1930, 1950-58).

10 — Ni namba ya dakika zilizobaki katika muda wa nyongeza  kwenye mchezo wa fainali ya mwaka 2006 nchi Ujerumani wakati Zinedine Zidane wa Ufaransa alipoamua kumpiga kichwa beki wa Italia, Marco Materazzi na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

11 — Ni muda ambao mshambuliaji wa Uturuki, Hakan  Sukur alifunga bao katika sekunde 11 dhidi ya Korea Kusini mwaka 2002, ndio bao la mapema zaidi kwenye historia ya Kombe la Dunia.

12 — Idadi kubwa ya mabao yaliyofungwa kwenye mechi moja  katika historia ya Kombe la Dunia wakati Austria ilipocheza dhidi ya Uswisi fainali za mwaka 1954, iliposhuhudia jumla ya  mabao 12 yakifungwa katika mchezo huo ambao Austria ilishinda 7-5.

13 — Ni idadi ya timu zilizoshiriki kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia mwaka 1930 nchini Uruguay.

14 — Idadi ya mabao yaliyofungwa na nyota wa Ujerumani, Gerd Muller alishikilria rekodi kwa muda mrefu ya kuwa kinara wa ufungaji kwenye Kombe la Dunia.

15 — Ni idadi ya mabao ambayo yamefungwa na mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo kwenye fainali tatu za Kombe la Dunia alizocheza mwaka (1998, 2002 na 2006).

                                                                Ronaldo

16 — Mwamuzi wa Russia, Valentin Ivanov alitoa kadi za njano 16 kwenye mchezo mmoja na kuweka rekodi hiyo, kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Dunaia mwaka  2006, Ujerumani mechi kati ya Ureno dhidi ya Uholanzi.

17 — Umri wa ambao gwiji wa Brazil, Pele alikuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza Kombe la Dunia na kufunga bao,  mwaka 1958 nchini Sweden.

18 — Mchezaji wa England, Geoff Hurst ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu kwenye fainali, bao lake kwanza kati ya matatu aliyoyafunga dhidi ya Ujerumani  Magharibi mwaka1966, alifunga dakika 18.

19 — Lucien Laurent aliifungia Ufaransa bao dakika ya 19 dhidi ya Mexico mwaka 1930, na kuwa mchezaji wa kwanza  kufunga bao kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia.

20 — Brazil 2014 ni fainali za 20 za Kombe la Dunia.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment