Misri imeomba mtandao wa kijamii
wa You Tube kuondoa video ya mwanamke akinyanyaswa kimapenzi katika
mkutano wa kisiasa Cairo,kumuunga mkono rais aliyechaguliwa hivi majuzi.
Msemaji wa rais Abdul Fattah al-Sisi alisema ombi hilo lilitolewa na ubalozi wa Misri mjini Washington.
Mwathiriwa alimuomba Bw.Sisi kuondoa video hiyo alipomtembelea hospitalini.
You tube bado haijaitikia ombi hilo la kuondoa kanda hiyo.
Video hiyo ambayo inaonyesha mwanamke akivuliwa
nguo hadi kuwa uchi na kushambuliwa eneo la Tahrir square, ilienea
mitandaoni mapema wiki hii.
Mfululizo wa mashambulizi wakati wa sherehe hizi za hivi majuzi yamelata vurumai.
Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na
serikali kilionyesha rais akiomba msamaha katika hospitali ya jeshi
Cairo, kutoka kwa mwathiriwa ambaye hakutajwa.
Mwanamke huyo alionekana akimuomba Bw. Sisi kuondoa video hiyo ya matukio hayo kutoka kwa mtandao uliokuwa ukiisambaza.
"Mwanangu anazimia kila mara anapoiangalia,"alinukuliwa akisea mwanamke huyo.BBC
No comments:
Post a Comment