Facebook imekuwa ikizua gumzo kuhusu sera na masharti yake ya kuweka picha kwa wanaotumia mtandao huo.
Hivi karibuni, ilikosolewa kwa kuondoa picha ya
wapenzi wawili wa jinsia moja wakibusiana , baada ya mtu kusema kuwa
picha hizo ni za kukera.
Lakini swala la hivi karibuni ambalo limejadiliwa sana kuhusiana na
picha kwenye mtandao huo wa kijamii, ni kuhusu mama mmoja aliyekuwa
akimnyonyesha mwanawe hadharani na kuweka picha hiyo kwenye akaunti
yake.
Baadhi walisema picha hiyo ilikuwa ya uchi mno na kwamba iliwakera watu wengi sana.
Sasa hivi Facebook imebadilisha sheria zake kuhusu picha za wanawake wakiwanyonyesha watoto wao.
Katika sehemu ya mtandao huo , maagizo sasa
yanasema kuwa ''Ndio tunaruhusu picha za wanawake wakiwanyonyesha watoto
wao ni jambo zuri na ambalo hatuwezi kulikosoa. Ni vyema kujua kuwa ni
muhimu kwa akina mama kuonyesha watu picha hizo kwenye Facebook. Picha
hizi sasa zinaruhusiwa.''
Facebook inasisitiza kuwa mabadiliko yoyote
wanayofanyia sera zake kuhusu picha, hutokana na malalamiko ya watumiaji
wa mtandao huo.
Katika nchi nyingi za Ulaya, wanawake wengi
huogopa kunyonyesha hadharanai kutokana na unyanyapaa. Wanawake nchini
Uingereza waliwahi kuandamana wakipinga unyanyapaa unaojitokeza kwa
wanawake ambao hunyonyesha watoto wao hadharani.
Swala la kuwanyonyesha watoto hadharani sio hoja
kwa wanawake wengi barani Afrika kwani kwao pale ambapo mtoto analilia
Titi mama hutafuta mahala safi na kumnyonyeshea mtoto wake.
Nini maoni yako kuhusu swala la kumnyonyesha mtoto hadharani?BBC
No comments:
Post a Comment