MUME wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa
miaka 17 (jina lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat
Gwajima amuachie mke wake, yaani Flora.
Akizungumza kwa machungu kwa njia ya simu kutokea alikojihifadhi huku
akionesha waziwazi hasira juu ya hisia zake, Mbasha alisema:
“Nimesika mke wangu baada ya matatizo yetu amehamia nyumbani kwa
Gwajima. Nataka mumwambie Gwajima aniachie mke wangu, mbona ananifanyia
hivyo?”
KINACHOMSHANGAZA
Mbasha ambaye mpaka sasa hajulikani alipo, aliendelea kudai kwamba
kinachomshangaza zaidi ni kwamba, Flora amekiuka utamaduni wa Kiafrika,
kwamba kama mke na mume wamegombana kiasi cha kushindwa kuishi nyumba
moja, mke anakwenda kwao lakini hilo la Flora kukimbilia kwa Gwajima
ndilo la ajabu zaidi kwake.
“Kama kweli Flora ameshindwa kuishi nyumbani kwetu (Tabata-Kimanga) kwa
nini asiende Morogoro kwa mama yake. Au kwa nini asirudi Mwanza kwenye
chimbuko la familia ya mzee Moses Kulola?
“Yeye badala yake amechukuliwa na Gwajima na kwenda kuishi naye nyumbani
kwake. Mimi sijapenda, sijapenda na sitapenda kamwe,” alisema Mbasha.
ATUHUMU MTOTO KULIPIWA ADA YA SHULE
Akiendelea kutoa la moyoni, Mbasha alituhumu kuwa mke wake kwa sasa ana
pesa nyingi licha ya kwamba wakati matatizo ya yeye kutuhumiwa kubaka
yanatokea na kuingia mitini alimwacha hana kitu.
Anasema: “Wakati matatizo yanatokea Flora nilimwacha mweupe. Mtoto wetu
(Elizabeth) alitakiwa kupelekwa shule, kwa hiyo ina maana hakwenda.
“Sasa nasikia mtoto amelipiwa ada na anakwenda shule. Nani kamlipia ada
mwanangu kama si Gwajima? Mimi naumia sana, kwa nini iwe hivyo? Kama
Gwajima ameamua mke wangu kukaa kwake kwa ajili ya kumsaidia kipindi
hiki cha matatizio ajue mimi sijapenda.
“Yeye Gwajima ana mke wake, najua hawezi kusema kitu kwa sababu Gwajima ni kila kitu lakini sijapenda.”
GWAJIMA SASA
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu
ambapo alisema hataweza kuzungumza kwa sababu yupo Mikumi akielekea
Dar.
Uwazi: “Sawa, lakini inadaiwa Flora yupo kwako. Hata jijini Dar habari
zimeenea kwamba yupo kwako. Mbasha mwenyewe pia amesema mke wake yupo
kwako. Unasemaje kuhusu hili?”
Gwajima: “Flora hakai kwangu na wala sijui alipo. Hao wanaosema anaishi kwangu si wa kweli. Hata mkija kwangu hamtamkuta Flora.”
UWAZI LAMSAKA FLORA
Uwazi lilianza kuingia mitaani kumsaka mwimbaji huyo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya kiintelejensia.
Ilikuwa kazi kubwa sana iliyoanza saa mbili na nusu asubuhi ya Jumapili
na ilipofika saa tano, Flora alipatikana kwenye hoteli moja (jina
tunalo) iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Alikuwa akijiandaa kwenda kanisani ikabidi hekima zitumike ili aweze kutoa dakika ishirini tu za mahojiano ambapo alikubali.
KUMBE ULIANZA UGOMVI
Akizungumzia kuhusu ugomvi katika ndoa na tuhuma ambazo mumewe anadai kuhusika nazo, Flora alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sina ugomvi na mume wangu Mbasha ninampenda sana ila ninamshangaa kutoa taarifa yetu ya ndani katika vyombo vya habari.
“Nimeshtushwa sana na kitendo hicho kwani kama ingekuwa ni ugomvi
baina yake na mimi tungekaa chini na kuyamaliza kama wanandoa. Siamini
kama njia hii anayoitumia italeta suluhu, bali itaendeleza matatizo.”
KUHUSU MADAI YA UBAKAJI
“Nakumbuka ilikuwa asubuhi ya Ijumaa ya wiki mbili zilizopita, Ima
(Emmanuel) aliniambia nijiandae kwenda ofisini kwetu kuangalia shughuli,
alinipitisha ofisini kisha yeye akarudi nyumbani.
“Baadaye alinipitia ofisini kurudi nyumbani. Nilimkuta binti
mlalamikaji akiwa hana raha na hali siyo nzuri, nilimuuliza tatizo ni
nini hakuniambia.
“Ilipofika Jumapili nilimwambia mume wangu twende kanisani lakini
alikataa, nilimuomba ufunguo wa gari ili mimi niende na familia,
akagoma. Ndipo ugomvi ulipoanzia, nilimuuliza umekuwaje? Mbona uko
hivi? Au umechanganyikiwa? Alinijibu anataka aondoke aniache na
familia.
“Baadaye akabadilika, akasema hapana haiwezekani yeye akaondoka, bali mimi ndiyo niondoke.”
ATISHIWA KUCHINJWA
“Nilimuomba tuwaite watu wazima ili waje kutupatanisha, akaniambia nikiondoka kwenda kutafuta watu atanichinja.
“Niliamua kuachana naye, nilimpigia simu rafiki yangu mmoja aje anipitie
na gari kwenda kanisani, lakini huyo rafiki yangu alipita na
kuniambia kuwa amepata dharura hivyo asingenipeleka kanisani.
“Nikamrudia mume wangu na kumwambia mbona kama umerogwa? Akasema ndiyo
amerogwa, nikamwambia twende kanisani ukaombewe, akakataa. Matokeo yake
akanikaba shingoni mpaka nikashindwa kuongea.
Nikamwambia unaniua ndipo akaniachia.
“Nilichukua gari la watu na familia yangu tukaenda kanisani. Kufika
kanisani nilimweleza Mchungaji Gwajima tatizo lililonipata, akaniambia
nirudi tu nyumbani kama hali itakuwa mbaya ataangalia cha kufanya.
“Baada ya ibada nilimwambia mdogo wangu arudi nyumbani na watoto, mimi nikaenda kukaa mahali nikiwaza cha kufanya.”
BINTI AMPIGIA SIMU
“Ilipofika kesho yake (Jumatatu) nikapigiwa simu na yule binti akidai
anaondoka nyumbani kwa sababu shemeji yake amemdhalilisha sana.
Nilimwambia asiondoke kuna mtu atakwenda kumchukua mchana kumleta
nilipokuwa.
“Alipoletwa nilishangaa kumkuta katika hali ambayo hawezi kutembea
sawasawa. Nikamuuliza vipi? Ndipo akanielezea jinsi mume wangu
alivyomfanyia.”
BINTI AENDA HOSPITALI
Flora aliendelea kusema kuwa, binti mwenyewe aliamua kwamba anakwenda
hospitali kucheki afya. Akasindikizwa na mdogo wake Flora. Kule vipimo
vilionesha kweli aliingiliwa kimwili. Madaktari walimshauri aende
polisi.
“Ndipo akaenda polisi na kutoa maelezo na kuandikiwa faili ambapo mume wangu akawa anatafutwa.
“Mume wangu amekuwa akisambaza habari kwamba nina mwanaume sijui nani!
Hicho kitu hakipo. Hata mwaka jana nilikwenda Uingereza lakini tulikuwa
wote.”
KUHUSU KUWA NA PESA, MTOTO KULIPIWA ADA
Kuhusu madai kwamba mtoto amelipiwa ada, yeye hana pesa, Flora alisema:
“Pale kanisani waumini walipojua nina matatizo na mume wangu na sipo
nyumbani, walipitisha harambee ambapo niliweza kupata shilingi milioni
tisa ndiyo maana mtoto akaenda shule na mimi nikabaki na za matumizi
maana kila kitu kuhusu akaunti ya benki anakijua mume wangu.”
MBASHA AOMBA KESI IFUTWE
“Mume wangu aliniomba msamaha baada ya haya mambo kutokea, nimemsamehe.
Aliniomba nifute kesi polisi, nikamwambia si mimi niliyepeleka kesi
polisi. Mimi siwezi kumsaliti yeye, kwanza nampenda sana Mungu kisha
yeye.”
AKUTWA AMEVUA PETE YA NDOA
Uwazi lilimkuta Flora akiwa hana ile pete ya ndoa iliyozoeleka kuwepo
kwenye kidole chake. Alipoulizwa alisema hakuna uhusiano wa pete
kutokuwepo kidoleni na ugomvi.
FAMILIA YACHAFUKA
Mwimbaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba ugomvi kati yake
na mume wake umesababisha familia kuchafuka maana umekuwa gumzo katika
kila kona ya mtaa.
GPL NA UDAKU
No comments:
Post a Comment