JUMLA ya watoto 863, wanaripotiwa kufanyiwa vitendo vya ulawiti huku wanaowafanyia hivyo wakiwa ni ndugu zao wa karibu.
Pia watoto 250 wametupwa na kutelekezwa huku 142 wakiwa wametekwa na 10 wamefanyiwa vitendo mbalimbali vya udhalilishaji.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo
cha Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, alipozungumzia Siku ya
Mtoto wa Afrika na changamoto mbalimbali zilizopo katika kulinda na
kuheshimu haki za watoto.
Kutokana na kukithiri kwa hali hiyo, ametaka haki na ulinzi wa mtoto
iwe ni ajenda ya kila mdau hasa wanasiasa kuifanya ya kitaifa katika
mikutano yao.
Sungusia alisema wanasiasa wanapaswa kufanya hivyo wakiamini kwamba
itahamasisha wananchi kwa uzito mkubwa kutokana na wao kuwa na nafasi
kubwa ya kusikilizwa na kuwafikia wananchi wengi kwa wakati.
Kwa upande wa serikali, alitaka iweke mikakati ya kiulinzi
itakayomwezesha mtoto kujitambua na kujilinda mwenyewe kabla ya mtu
mwingine.
Pia alitoa rai kwa wananchi na wanajamii kwa ujumla kuheshimu nafasi
ya watoto katika jamii na pale ambapo haki zao zinakiukwa basi ni vizuri
kutoa taarifa kwa vyombo husika.
“Matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za watoto yamekuwa yakitokea na
kuendelea kwa sababu taarifa hazitolewi, na hata pale zinapotolewa
kunakosekana ushahidi wa kutosha na hivyo kufanya watuhumiwa kuendelea
na matendo maovu,” alisema.
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Juni 16 ikiwa ni kumbukumbu
ya kupinga mauaji ya watoto wanafunzi waliokuwa wanaandamana kudai haki
ya usawa wa elimu na haki nyinginezo katika kitongoji cha Soweto,
nchini Afrika Kusini mwaka 1976.TANZANIA D
No comments:
Post a Comment