Pages

Tuesday, June 17, 2014

HABARI KWA UFUPI

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge, ameibua madudu makubwa kwenye bajeti ya mwaka 2014/2015 ambapo amesema ina pengo la sh trilioni 4.9 sawa na asilimia 24.Chenge alisema bajeti hiyo ina pengo la sh trilioni 2 ambazo hazikupatikana mwaka 2013/2014 na sh trilioni 1.6 zilizoongezeka mwaka 2014/2015 kutokana na kuongezeka kwa bajeti kutoka sh trilioni 18.2 hadi trilioni 19.8.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dk. Sikubwambo Ngendabanka, amesema matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ni janga la kitaifa linaloisababishia serikali hasara ya mabilioni fedha kutibu athari zake.

Jumla ya watoto 863, wanaripotiwa kufanyiwa vitendo vya ulawiti huku wanaowafanyia hivyo wakiwa ni ndugu zao wa karibu. Pia watoto 250 wametupwa na kutelekezwa huku 142 wakiwa wametekwa na 10 wamefanyiwa vitendo mbalimbali vya udhalilishaji.

Marekani imetangaza kuwa inatuma wanajeshi 275 nchini Iraq kusaidia kulinda maafisa na Ubalozi wake mjini Bagdad.Tangazo hilo limetolewa wakati maafisa wa Marekani na Iran wakifanya mazungumzo kuhusu hali nchini Iraq katika kongamano linalojadili maswala ya nyuklia mjini Viena.

Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba.Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.


No comments:

Post a Comment