Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya
mashambulizi hayo na kuambia shirika la habari la Reuters kuwa
operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi
yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia
hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde.BBC
No comments:
Post a Comment