Pages

Thursday, June 19, 2014

HABARI KWA UFUPI



Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amewataka wakulima, wafugaji kuipiga mawe Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutenga sh bilioni 50 kwa ajili ya safari za rais huku ikitenga sh bilioni 51 kwa maendeleo ya kilimo.


Wakati baadhi ya watu wakiamini wabunge hulipwa zaidi ya sh milioni 10 kwa mwezi, mmoja wa wabunge wa Bunge la Muungano, amejikuta akitoka na mshahara wa sh 50,000 kwa mwezi, Tanzania Daima limebaini.

Kamishina wa Polisi Jamii nchini, Musa Ally Musa, amepiga marufuku Polisi Jamii kutumia silaha za mapanga katika ulinzi badala yake watumie filimbi.Musa alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kutokana na changamoto iliyopo kwa jamii, ya kutokuelewa maana ya Polisi Jamii kunachangia polisi hao kuonekana kama majambazi.

Iraq imeomba rasmi usaidizi wa Marekani kushambulia kwa ndege wapiganaji wa kiislamu walioteka miji kadhaa nchini humo wiki hii. Awali wapiganaji hao wa madhehebu ya Sunni walishambulia kiwanda kikubwa zaidi cha kusafishia mafuta nchini Iraq katika mji wa Baiji kaskazini mwa Baghdad.

Mtaalamu mashuhuri wa maradhi ya Ki-akili ya dementia ambayo huathiri uwezo wa kufikiri, Daktari Dennis Gillings, amejitokeza na kuzungumzia kile anachokiita, mwendo wa Kobe katika taratibu ya kupata tiba mpya ya ugonjwa huo. Ugonjwa huo wa akili unawaathiri zaidi ya watu milioni 4 kote Duniani.

Kitengo cha utendakazi cha askari polisi Nchini Kenya kimekumbwa na shida ya ukosefu wa makazi.Hali imekuwa mbaya sana katika ski za hivu punde kiasi ya kuwa maafisa wa kike na wenzao wa kiume, wamelazimika kutumia kwa pamoja vyumba vyao vichache.

No comments:

Post a Comment