Mabingwa watetezi wa kombe la
dunia, Uhispania wameondolewa kutoka kwenye mchuano ya kombe la dunia
mwaka 2014, huko Brazil baada ya kushindwa mabao 2-0 na timu ya Chile.
Matokeo hayo yaliiwacha mabingwa hao watetezi wakiwa wa mwisho na bila alama yote katika kundi B.
Chile pamoja na Uholanzi wanafuzu katika raundi ya pili.
Kufuatia ushindi huu wa mabao 2-0 mikononi mwa
Chile mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania sasa wamehakiki
tikiti za ndege kurejea nyumbani pamoja na Australia .
Hii ni baada ya Uholanzi kushinda mechi yake ya pili na kuongoza kundi B ikiwa na alama 6 sawa na Chile.
Chile na Uholanzi hata hivyo zitakutana katika mechi ya kuamua yupi kati yao ataongoza kundi hilo.
Mshindi wa pili katika kundi B atachuana na
bingwa katika kundi A inayojumuisha wenyeji Brazil na washindi wa pili
katika kundi hilo Mexico.
Kwa upande wao Uhispania ambao sasa wamefungwa
jumla ya mabao 7 watachuana na Australia katika mechi ambayo haitakuwa
na umuhimu wowote .
Uholanzi waliishinda Uhispania kwa mabao 5-1, katika mechi ya kwanza, na baada ya mechi hii ya pili, Uhispania wanabakia bila ushindi wowote wakiwa wamefungwa mabao saba katika michuano miwili ya kombe la dunia mwaka 2014.
Hii ndio mara ya kwanza janga kama hili kuifanyikia timu ya Uhispania katika michuano ya soka ya kombe la dunia.
Chile walikua na nafasi mbili za kufunga mabao kabla hata mechi hiyo kuchukua dakika mbili.
Alexis Sanchez alianza mashambulizi ya Chile na kuisumbua safu ya ulinzi ya Uhispania.
Pasi yake safi ilimpata Eduardo Vargas ambaye shuti lake lilitoka nje baada ya kuguswa na mchezaji wa Uhispania.
Sergio Busquets alishindwa kuidhibiti kona iliyofwatia naye Gonzalo Jara akawa karibu na kuugonga mpira kwa kichwa ambao ulitoka nje hatua chache tu nje ya lango.
Uhispania ilikua imeishinda Chile matatu kwa moja katika michuano yao kumi ya awali, bila kushindwa.
Hata hivyo, timu hiyo ya mkufunzi Jorge Sampaoli, iliwapa wachile bao ambalo hata wahispania wenyewe wangependezwa nalo.
Sanchez na Arturo Vidal walipenya katika kiungo cha kati cha Uhispaniana kumpa pasi Charles Aranguiz katika eneo la hatari la Uhispania.
Bao hili bila shaka linafaa kuwa bao zuri la ushirikiano baina ya wachezaji wa timu, katika michuano hii.
Alonso na Diego Costa walijaribu kushambulia ila mashambulizi yao hayakufua dafu kuiokoa hali ya kutatanisha ya La Furia Roja.
Matarajio ya mashabiki wa Uhispania yalizidi
kudidimia wachezaji wa Chile walivyozidi kuwazuia vijana wa kikosi cha
Vincente Del Bosque.
Kwa kiutani, wachezaji wa Chile walionekana
kuiga mtindo mzuri wa pasi wa wahispania TIKI-TAKA na pia kuhakikisha
wahispania hawauupati mpira.
Kosa la Xabi Alonso lilisababisha kufungwa kwa bao la pili.
Mkwaju wa Sanchez ulitemwa na Casillas na ukamrudia Aranguiz ambaye hakusita kuurudisha kimiani .
Costa angeweza kufunga bao baada ya muda wa
mapumziko alipopewa pasi na Andres Iniesta na kumwacha akiwa moja kwa
moja na kipa wa Chile Claudio Bravo.
Costa alishindwa kuudhibiti mpira na ukachukuliwa na Mauricio Isla.
Sergio Busquets na Sergio Ramos walifanya mashambulizi mengine lakini ulinzi wa Chile ulilidhibiti lango lao.
Chile walionekana kuchoka katika dakika za
mwisho za mechi hiyo, hata hivyo waliweza kuhimili mashambulizi ya
wahispania na kuisumbua safu ya ulinzi ya wahispania pia.
23:54 Mechi imekamilika Uhispania 0-2 Chile
23:49 Dakika 6 za ziada zitachezwa kuamua iwapo Uhispania wataiacha kombe la dunia Brazil na kurejea nyumbani mapema
23:49 Uhispania 0-2 Chile
23:48 Dakika 3 za mwisho matokeo bado ni yaleyale ya kipindi cha kwanza
23:47 Bravo anaudaka bila wasiwasi
23:47 Freekick Kuelekea lango la Chile.
23:43 Iniesta anamlazimu Bravo kuutema nje mkwaju wake na ni Kona kuelekea Chile
23:42 Australia na Uhispania hawajashinda mechi yeyote Brazil 2014
23:41Kufuatia matokeo ya mechi iliyotangulia Uholanzi inaongoza kundi B ikiwa na alama 6 huku Chile ikiwa na alama sawa na hizo
23:40 Uhispania inachini ya dakika 10 sasa kufunga mabao mawili amawajipange kuabiri ndege ya kurejea nyumbani
23:30 Mwaka wa 2010 Italia walitua Afrika Kusini lakini wakashindwa katika hatua ya makundi
23:29 Mabingwa wa tiki taka wanafunzwa mfumo mpya wa soka na Chile
23:26 Andrés Iniesta anakosa kuitumia ipasavyo nafasi hiyo
23:26 Freekick Francisco Silva (Chile).
23:23 Fernando Torres anaingia , Diego Costa anapumzishwa
23:19 Fernando Torres anajianda kuingia kocha
Del Bosque akitafuta uokozi katika mechi hii zikiwa zimesalia dakika 30
pekee ya mechi hii
23:16 Uhispania 0-2 Chile 56''
23:15 Uhispania wanakodolea jicho safari ya kurudi nyumbaniiwapo mechi hii itamalizika hivi ilivyo
23:12 Sergio Ramos anapoteza nafasi ya kuinusuru dau lao anapopiga nje mpira
23:12 Freekick kuelekea lango la Chile
23:11 Koke anaangushwa mbele ya lango
23:10 Mauricio Isla anaupoteza mpira huku Uhispania ikifanya mashambulizi.
23:08 Diego Costa anakosa nafasi mbele ya lango la Chile inakuwa Kona lakini inazuiliwa na safu ya ulinzi ya Chile
23:04 Kipindi cha pili kinaanza katika mechi hii ya kihistoria kati ya Chile na Mabingwa watetezi Uhispania
23:03 Koke anajiandaa kuingia katika ile nafasi iliyokuwa imechukuliwa na Xavi Alonso
22:45 Hii ndiyo itayokuwa mara ya kwanza kwa bingwa mtetezi kushindwa katika mechi mbili za kwanza za kombe la dunia .
22:45 Iwapo mechi hii itakamilika ilivyo sasa ,Uhispania watakuwa hawana budi ila kuelekea nyumbani
22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika.
22;44 UHISPANIA 0-2 CHILE
22:44 Uhispania inafungwa bao la pili kutokana na mkwaju wa Charles Aranguiz
22:43 GOOOOOOOAL
22:42FREEKICK kuelekea upande wa Uhispania unatemwa na Cassilas
22:42 Mechi hii inachezewa katika nusu ya Uhispania huku chile ikiendeleza mashambulizi
22:40 Xavi Alonso anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea visivyo Isla
22:31 Iniesta anaupoteza mpira na sasa ni Freekick kwa upande wa Chile ambayo inachukuliwa kwa haraka .
22:30 Freekick kuelekea kwa lango la Chile
22:28 Refarii Mark Geiger anatoa kadi yake ya kwanza ya njano katika mechi hii kwa Vidal
22:27 Chile wanaanza nipe nikupe kati ya Sanchez na Mena
22:26 Diego Costa anafyatua mkwaju unaogonge upande wa nje wa neti
22:26 Kipa wa Uhispania Iker Cassillas awazomea walinzi wake kwa kuruhusu mashambulizi .
22:20 Eduardo Vargaz aipatia Chile bao muhimu dhidi ya mabingwa watetezi
22:19 Chile wanapata bao lao la kwanza kupitia kwa Vargaz dakika ya 19
22:19 GOOOOOOOAL
22:18 Chile inaendelea na mashambulizi kuelekea a Uhispania Bado mechi hii haijatulia
22:16 Goalkick kuelekea lango la Uhispania
22:14 Alonso anapoteza nafasi ambayo ni ya ana kwa ana na kipa wa Chile Bravo
22:13 Alonso anaupoteza mpira na kuonekana kumkera Del Bosque
22:13 Freekick Kuelekea lango la Chile inayopigwa na Alonso.
22:04 Kiti cha Kocha wa Uhispania Del Bosque kimekuwa moto tayari
22:03 Iker Cassillas anajikakamua na kuudaka bila wasiwasi.
22:02 KONA. kuelekea upande wa Uhispania
22:02 Mpira umeanza na Chile wanafanya shambulizi la mapema ambalo Alonso na Uhispania hawana jibu inakuwa ni Kona.BBC
No comments:
Post a Comment