Pages

Wednesday, June 11, 2014

HABARI KWA UFUPI


Watu watatu wa familia moja, akiwemo mwanafunzi wa sekondari, wameuawa kinyama kwa kukatwa mapanga shingoni na sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiojulikana.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2:30 usiku katika Kijiji cha Msungua, Kata ya Irisya, Tarafa ya Sepuka wilayani Ikungi wakati wanafamilia hao wakiwa wamelala ndani.


 Mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), amezua mjadala mkali bungeni kwa kuishambulia Serikali ya CCM akidai kuwa mawaziri wake wamekuwa wakitoa majibu mepesi yasiyo na mashiko.Mkosamali alitoa kauli hiyo jana wakati akiuliza swali la kuitaka serikali ieleze ni lini itapeleka muswada bungeni kwa ajili ya kutunga sheria ambayo itatoa nafasi ya kila mbunge kulindwa kisheria kama ilivyo kwa viongozi wengine.

 Wakati matumaini ya Tanzania kuandika katiba mpya baada ya miaka 50 ya uhuru, yakiwa yamefifia kutokana na ukigeugeu wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mitihani mitano inamkabili Rais Jakaya Kikwete ili kutanzua utata huo.

Uwezekano wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, kushinda cheo cha Urais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumeanzisha mjadala mkali nchini Uganda, huku wakereketwa wa haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda wakipinga asichaguliwe.

Wapiganaji wa Kiislamu wanadaiwa kuendelea na kuteka maeneo zaidi nchini Iraq, katika hatua ambayo Marekani imetaja kama ni tishio kwa eneo zima. Polisi wa Iraq wanasema kwamba muungano wa makundi hayo - Islamic State of Iraq na Levant - ambao wanajiita kwa pamoja ISIS wameteka mikoa ya Kirkuk na Salehddin.

No comments:

Post a Comment