Jeshi
la Polisi Zanzibar limesema bomu la kurushwa lililolipuka juzi katika eneo la
Darajani na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine saba ni la kivita
lililotengenezwa kiwandani.
Polisi
wamefanikiwa kumnasa mwanamke anayedaiwa kumtesa kwa kipigo na kumng’ata mtoto
Merina Mathayo (15), kumsababishia majeraha makubwa kichwani.Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura akizungumza jana alisema walifanikiwa
kumnasa juzi, mwanamke huyo akiwa mafichoni Mbagala wilayani Temeke.
Watu wanaoshukiwa
kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi na mahoteli na
vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .Makabiliano makali yameripotiwa sehemu
kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea maeneo ya msitu karibu na
kisiwa cha Lamu.
Vuguvugu
la Sunni lenye msimamo mkali la ISIS ambalo limeteka maeneo ya Kaskazini mwa
Iraq limesambaza picha ambazo zinaonyesha jinsi wapiganaji wake walivyoangamiza
idadi kubwa ya wanajeshi wa Iraq.
Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufaidi matumizi ya
teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika mechi ya kombe la dunia linaloendelea
huko Brazil.
No comments:
Post a Comment