Harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015
zimeanza. Polisi wameanza mafunzo yatakayowaongezea uwezo wa kusimamia uchaguzi
huo.Mafunzo hayo yanafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), kupitia mradi wake wa Uwezeshaji wa Demokrasia (DEP).
Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es
Salaam jana walikumbwa na taharuki baada ya kituo cha daladala cha Mwenge
kuhamishiwa eneo la Makumbusho .Mwananchi lililokuwa kwenye kituo hicho mapema
jana, lilishuhudia baadhi ya abiria wakistaajabu hali ya mabadiliko hayo ambayo
yalipokewa kwa shangwe na wakazi wa Makumbusho huku wale wa Mwenge wakipingana
na uamuzi.
Msanii
muigizaji kutoka Kenya Lupita Nyong'o ameteuliwa kuijiunga na mabingwa wengine
wa kimataifa katika filamu maarufu zaidi duniani STAR WARS.Lupita anatarajiwa
kuonekana katika kipindi cha saba msimu huu wa Star Wars.
Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja
wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa
shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za
kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
Zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka
Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wamefukuzwa kutoka Congo Brazaville tangu mwezi
Aprili.Wengi wao sasa wanaishi katika kambi za muda nchini DRC.
No comments:
Post a Comment