Msanii muigizaji kutoka Kenya Lupita Nyong'o
ameteuliwa kuijiunga na mabingwa wengine wa kimataifa katika filamu
maarufu zaidi duniani STAR WARS.
Lupita
anatarajiwa kuonekana katika kipindi cha saba msimu huu wa Star Wars.
Hii inafatia ufanisi mkubwa aliopata katika filamu '12 years a slave',
ambapo alinyakua taji la Oscars la muigizaji bora msaidizi.
Msanii mwingine aliyetajwa kujiunga na 'star
Wars' ni Gwendoline Christie,ambaye kwa sasa anatambulika zaidi katika
mchezo wa televisheni wa 'Game of Thrones' unao endelea kupata umarufu
duniani. Yeye pia ataonekana katika filamu ya 'Hunger Games'.
"Nashindwa kuelezea furaha yangu kwa Lupita na
Gwendoline kwa kujiunga na waigizaji wengine katika kipindi hiki cha
Star Wars.,'' amesema Kathleen Kennedy, rais wa kampuni ya Lucasfilm
inayosimamia utengezajiwa filamu hiyo.
Wengine waliotajwa
Waigizaji wengine wapya watakao jiunga katika
kpindi hicho ni John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac,
Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow. Wale wa awali tangu
mwanzo ni Harrison Ford, Carrie Fisher, Mark Hamill, Anthony Daniels,
Peter Mayhew, na Kenny Baker.
Star Wars: Kipindi cha VII inasimamiwa na J.J.
Abrams na kuelekezwa kuwa filamu baada ya kufanya vyema kama kipindi cha
televisheni kwa muda mrefu.
Filamu hiyo inatarajiwa kuwa tayari kuoneshwa katika sinema kuanzia tarehe 18 Disemba, 2015.BBC.
No comments:
Post a Comment