Wataalamu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Kanda ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wa hazina ya madini ya dhahabu
katika Mlima Rankiroga na Mto Karabaline katika Kijiji cha Mgongo, Kata ya
Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa Mark
Mwandosya, amefanya maamuzi magumu ya kuinusuru Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
kuanguka bungeni.Mwandosya ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi
Maalumu, alifanya maamuzi hayo juzi wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu hoja
nzito ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), aliyeitaka serikali kutangaza
tatizo la maji kuwa janga la kitaifa na kutangaza mpango kabambe wa kukabiliana
nalo.
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, imeingia katika kashfa nzito ya kudaiwa kutafuna zaidi ya sh milioni 200
za kujenga ukuta wa kuzuia kuanguka kwa jengo la lililokuwa Shirika la Uvuvi
nchini (Tafico) kutokana na mmomonyoko
unaosababishwa na maji ya bahari.
BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya
watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.Hii
inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya
200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.
Rais Barack Obama anatarajiwa kumteua balozi wa
kwanza wa Somalia, mara ya kwanza tangu nchi hiyo itumbukie katika vita vya
wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miongo miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment