Mwanamke mmoja nchini Kenya
ameamrishwa na mahakama kumlipa mumewe shilingi elfu tatu au dola 35
kama hela za kukidhi mahitaji yake na watoto wake kila mwezi.
Mwanamke huyo kwa jina Roselyn Muyonga, ambaye
anatuhumiwa kwa kuwatelekeza mumewe na watoto wake watatu , huenda
akafungwa miezi mitano jela au kutozwa faini ya shilingi laki mbili
ikiwa atakosa kutekeleza amri ya mahakama.
Mwanamume huyo hufanya kazi za kibarua.
Afisaa mmoja wa watoto katika jimbo la Kakamega
Magharibi mwa Kenya, alisema kuwa mwanamke huyo alipuuza jukumu lake la
kulea watoto wake baada ya yeye na mumewe kutalakiana.
Afisa huyo alisema kuwa wanaume huachiwa
majukumu mengi sana wakati wanapoachwa na watoto na kwamba wanawake kama
Roselyn wanapaswa kuamrishwa kuwatunza watoto wao hata kama wameachana
na waume zao.
Tayari mashirika kadhaa yanataka kushinikiza
sheria ya kuwashurutisha wanawake kutoa mchango kwa kuwalea watoto wao
wanapoachana na mwanamume au baba ya watoto.
Kwa mujibu wa afisaa mmoja wa watoto, visa vya wanawake kuwatelekeza watoto wao katika jimbo hilo vimeongezeka.BBC
No comments:
Post a Comment