Maafisa wa afya duniani
wanaarifu kuwa watu wasiopungua 208 wameaga dunia kutokana na virusi vya
Ebola nchini Guinea baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa siku za hivi
karibuni.
Angaa watu 21 waliaga dunia na visa vingine 37
vinavyohusiana na Ebola kuripotiwa kati ya tarehe 29 mwezi Mei na tarehe
1 mwezi Juni na kufikisha idadi ya visa hivyo kufikia 328 katika taifa
hilo lililoko magharibi mwa Afrika.
Kati ya visa hivi, 193 vilithibitishwa kupitia vipimo vya maabara.
Hadi sasa, hakuna dawa za kuzuia wala kutibu Ebola- moja kati ya virusi hatari sana duniani.
Zaidi ya nusu ya vifo vya hivi karibuni vilitokea kusini mwa eneo la Guekedou, mahali ambapo ugonjwa huo ulianzia.
Visa vitatu vimedhibitishwa na vingine 10 vinavyodhaniwa kuwa wa ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi Jirani ya Sierra Leone.
No comments:
Post a Comment