Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.
Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya
utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa
kumfikisha katika ushindi huo.
Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina
'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube
tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa
aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu
Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida.BBC
No comments:
Post a Comment