Pages

Friday, June 06, 2014

HABARI KWA UFUPI



Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.


Kasi ya ongezeko la wageni wanaoingia na kufanya shughuli za kiuchumi mkoani Rukwa imetajwa kwamba ndiyo kiini cha kushamiri kwa biashara ya ngono, hivyo kusababisha ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Kampuni za simu za mkononi za Tigo, Airtel na Zantel zimeunganisha huduma zao za kutoa, kutuma na kuweka fedha na sasa mteja anaweza kutuma fedha kutoka mtandao mmoja kupitia mwingine.

Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.

Kwa mara ya kwanza Misri imepitisha sheria inayotaja unyanyasaji wa wanawake kuwa uhalifu.Chini ya sheria hiyo wanaume watafungwa miaka 5 gerezani kwa kuwanyanyasa wanawake hadharani au faraghani.Sheria hiyo imepitishwa kama hatua ya mwisho kuchukuliwa na rais anayeondoka wa Misri Adly Mansour.

No comments:

Post a Comment