Kampuni ya ufuaji
umeme ya IPTL, imesema dhamira yake ya kushusha bei ya umeme kwa Watanzania ipo
palepale.Katibu na mshauri wa masuala ya sheria wa kampuni hiyo, Joseph
Makandege, alieleza hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi
wa habari.Makandege alisema licha ya kuwepo kwa maneno mbalimbali dhidi yao,
hawana muda wa kulumbana na badala yake wanachapa kazi, ili kuhakikisha malengo
waliyojiwekea wanayafikia.
Daktari wa
Hospitali ya Nyamagana, Raymond Simon (36), mkazi wa Nyamagana, Mwanza
aliyekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Nesta Inn iliyopo
Ubungo, Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura,
alisema jana kuwa pembeni mwa mwili wa daktari huyo kulikutwa bomba la sindano
lililokuwa na masalia kidogo ya damu na kete moja ya vitu vinavyodhaniwa
ni dawa ya kulevya.
Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amemvaa Rais Jakaya Kikwete kuwa ni
mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza kuchochea jeshi lake kufanya
mapinduzi ya kijeshi ili kuzuia matakwa ya wananchi juu ya katiba mpya
kutekelezwa.
Viongozi kumi na watatu wa mataifa na mamia ya
wafanyabiashara wanakutana Abuja kwa mkutano wa biashara na masuala ya uchumi
duniani kuhusu Afrika.Mkutano huo mwaka huu ulikuwa ni fursa kwa Nigeria baada
ya kutajwa kuwa nchi yenye uchumi mkubwa Afrika, lakini mashambulio ya kundi la
wapiganaji wa Boko Haram na wasiwasi wa kiusalama yameugubika mkutano huo.
Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Urusi, Vladimir
Putin, ametoa wito kwa makundi yanayotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi
Kusini Mashariki mwa Ukraine waahirishe kura ya maoni ya Jumapili juu ya kutaka
kujitenga kama hatua muhimu kuimarisha mashauriano ya amani kati ya makundi
yanayozozana nchini humo.
No comments:
Post a Comment