Mkazi wa kitongoji cha
Nyaruhande,wilayani Bariadi anatafutwa na Polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake
baada ya kumcharaza fimbo sehemu mbalimbali mwilini.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Simiyu,Charles Mkumboalimtaja mtoto aliyefariki kuwa ni Sumayi Ndulu
(12),anadaiwa kupigwa kichwani
,tumboni,mbavuni na kuchomwa kisu mkononi.
Mkumbo alisema baba huyo anadaiwa
kumpiga mtoto huyo baada baada ya kurudi kutoka kwenye pombe na kukuta
ameandaliwa chakula tofauti.
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni
kipigo kutokana na mtoto kwenda kwa babu yake Bululu bila kuaga.Mama mzazi wa
mtoto huyo,Kwandu Mboje (30),alidai mumewe ana tabia ya ulevi na walitengana
kutokana na kumpiga mara kwa mara bila kuwa na makosa.Alisema baada ya kugundua
kuwa mtoto amekufa,alimbeba na kwenda kumtupa kwenye dimbwi la maji ili
kupoteza ushahidi.
No comments:
Post a Comment