Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka
wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa'
na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.
Wanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu
kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi
kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya
baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea
wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo
kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya
maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Viumbe hawa wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa
kushikiliwa na mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki
ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara
na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya
sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo
za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012
kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano
ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi
wa Marekani na Uingereza.
Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.BBC
No comments:
Post a Comment