Pages

Tuesday, May 13, 2014

INATISHA.......MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YANAZIDI KUPANDA




Maambukizi ya virusi vya Ukimwi  (VVU)wilaya ya karagwe yameongezeka kutoka asilimia 4.8 mwaka jana hadi 5.8 mwaka huu,huku maambukizi ya mkoa yakiongezeka kutoka asilimia 3.4 kufikia 4.8.
Akisoma risala ya utii kwa Rais kwa kiongozi wa mbio za mwenge hivi karibuni,Mkuu wa Wilaya ya Karagwe,Dary Rwegasira alisema maambukizi hayo yamepanda kutokana na mila potofu na biashara ya ukahaba kwa baadhi ya wananchi.

No comments:

Post a Comment