Kampuni mbili za Kenya zimeingia katika mzozo kuhusu
usambazaji wa kazi za msanii nyota wa muziki wa Injili wa Tanzania Rose Muhando
imefahamika.Katika miaka kadhaa iliyopita kumekuwepo na msuguano kati ya Rose
Muhando na wasambazaji wa muziki wa Kenya ambao wana haki ya kusambaza muziki
wake nchini humo.
Hata hivyo inadaiwa kuwa kampuni nyingine ya Kenya ilikwenda Tanzania kwa siri ilisaini mkataba na mwanamuziki huyo hivyo kuzusha mgogoro katika mchakato huo.
Alipofuatwa Kassanga alithibitisha kuwa ni kweli lakini kwamba pande zote zinahusika kwa sasazinafanyia kazi njiaya kutatua tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment