Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini, Diamond Platnum ameahidi
makubwa kwa mashabiki wake wa Mtwara katika onesho litakalofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Makonde Club, mjini humo.
Katika shoo hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki, Diamond
aliyefanikiwa kujizolea mashabiki wengi, atasindikizwa na kipenzi chake
Malkia wa Bongo Movie, Wema Sepetu.
Akizungumza juzi katika ofisi za Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini
wa tamasha hilo, Diamond amewasihi wapenzi na mashabiki wake kukaa mkao
wa kiburudani kwani amejiandaa vizuri kufanya makubwa.
“Mashabiki wote waliopo Mtwara watashuhudia nikiimba live nyimbo
yangu mpya ya ‘My Number One remix’ niliyomshirikisha Davido kutoka
nchini Nigeria.
“Huwa sipendi kuwaangusha mashabiki zangu, hivyo basi nawaahidi
makubwa sana katika tamasha hilo na ningependa kuwaona wengi
wakihudhuria show hiyo kwani kutakuwepo na mengi ambayo hawakutarajia
kuyaona,” alisema Diamond.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin
Twissa, alisema wanajivunia kudhamini tamasha hilo la aina yake.
“Tunaahidi kuendelea kuwaunga mkono wasanii wetu wa Kitanzania na
kujivunia kilicho chetu, wote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumekuwa
msitari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wetu na tutaendelea na jitihada
hizo na kufikia viwango vya wasanii wengine wa kimataifa,” alisema.Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment