Daktari wa Hospitali ya Nyamagana, Raymond Simon
(36), mkazi wa Nyamagana, Mwanza aliyekutwa amekufa katika nyumba ya kulala
wageni iitwayo Nesta Inn iliyopo Ubungo, Dar es Salaam.Kamanda wa
Polisi Mkoa
wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema jana kuwa pembeni mwa mwili wa daktari
huyo kulikutwa bomba la sindano lililokuwa na masalia kidogo ya damu na kete
moja ya vitu vinavyodhaniwa ni dawa ya kulevya.
Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kwa uchunguzi.
Katika hatua nyingine, Kauma Kayima anayesadikiwa
kuwa mgeni kutoka Hong Kong, amekutwa amekufa
katika nyumba ya kulala wageni
iitwayo Euro Lodge iliyopo Sinza.
Kamanda Wambura alisema sababu za kifo ilielezwa
marehemu alikuwa akilalamika anaumwa kichwa.
Maiti imehifadhiwa Hosipitali ya Taifa ya
Muhimbili.
No comments:
Post a Comment