Pages

Tuesday, April 29, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI





Meneja wa Benki ya  Barclays Tawi la Kinondoni,  Alune Kasililika (28), anadaiwa kuchonga mpango wa majambazi kuvamia na kisha kupora kiasi kikubwa cha fedha katika  tawi hilo.Katika tukio hilo lililotikisa
Jiji la Dar es Salaam kwa takriban wiki tatu zilizopita, majambazi hao kwa kushirikiana na meneja huyo, wanadaiwa kuchota sh milioni 390. 2, dola za Marekani 5,5000, euro 2,150 na paundi 50.

Harakati za kujiimarisha za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) sasa zinatarajiwa kuhamia kwenye Bunge la Bajeti litakaloanza vikao vyake Mei 6, mwaka huu.UKAWA kesho wanatarajia kufanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar, kueleza wananchi sababu za kususia vikao vya Bunge la Katiba lililoahirishwa wiki iliyopita.

Jaji wa mahakama nchini Misri, amewahukumu kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie.Mawakili wa watuhumiwa wanasema kuwa wateja wao walikabiliwa na makosa mengi yakiwemo, kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka 2013 ambapo polisi mmoja aliuawa.

Muda wa mwisho uliowekwa na Marekani wa mpango wa mashariki ya kati umemalizika.Mchakato huo unaonekana kugonga mwamba . Israeli na Palestina wamekataa kuendelea na mazungumzo zaidi.Mazungumzo yao yalivunjika pale Israeli ilipoukataa mpango wa amani baina ya makundi makuu mawili ya Wapalestina wa kuunda serikali ya Umoja na hasira ya wapalestina kutokana na ujenzi wa Israeli wa makazi mapya katika maeneo yanayokaliwa .

No comments:

Post a Comment