Mwanamuziki mwenye asili ya Uingereza anafaya kazi zake
nchini Marekani ,Rita Ora almanusura ampige kibao mtangazaji wa redio
aliyemuuliza kuhusu usiano wake na Jay Z.
Akiwa katika mahojiano na kituo cha redio cha Power 105
fm,mtangazaji wa kipindi cha asubuhi DJ alimuuliza Charlamagne alimuuliza Rita
iwapo ana uhusiano wa kimapenzi na Jay Z.
Mwanamuziki huyo aliamka
na kutoka kwenye kiti na kutaka kumpiga kibao mtanzaji huyo huku akisema
“Huwezi kumvunjia heshima Beyonce kiasi hicho.Usirudie tena”mtangazaji huyo
alijitetea akisema hayo siyo maneno yake,bali tetesi ambazo zimezagaa mitaani
kuwa uhusiano wao ni zaidi ya ule wa kikazi.
Hata hivyo watangazaji wengine walifanikiwa kumtuliza Rita
ambaye alikubali kuendelea na mahojiano hayo,lakini kwa sharti la kutoendelea
kuzungumzia swala la Jay Z kwa sababu ni kumkosea Beyonce.
Rita Ora anafanya shuguli za Muziki nchini Marekani akisimamiwa
na Jay Z,katika Kampuni yake ya Roc Nation.
No comments:
Post a Comment