Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, amewaagiza makamishna na wakurugenzi wa sekta ya afya kuweka sera ya
wafanyakazi kupima afya mara kwa mara.Alitoa agizo hilo mjini hapa mwishoni mwa
wiki kwenye baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, ametoa msamaha kwa
wafungwa 3,967.Ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara
ya 45(1) ya Katiba ya Muungano ya sasa.Katika taarifa iliyotolewa jijini Dar es
Salaam jana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais Kikwete amewasamehe
wafungwa hao walikuwa katika makundi yafuatayo:
Waandishi wa habari nchini wanatarajiwa
kuungana na wenzao duniani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani (WPFD), yanayotarajiwa kufanyika Mei 2-3.Akitangaza sherehe hizo
jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya habari
Kusini mwa Jangwa la Sahara (MISA), Mohammed Tibanyendera, alisema maadhimisho
hayo yatakayowashirikisha washiriki zaidi ya 200 yatafanyika jijini Arusha.
Mahakama moja katika mji wa
Minya leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu hukumu ya kifo
iliyotolewa mwezi uliopita kwa wafuasi 529 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood
ambalo sasa limepigwa marufuku nchini humo.Kesi hiyo ilizua shutuma kali kutoka
jamii ya kimataifa.
Mmoja wa wachunguzi wa muungano
wa Ulaya waliokamatwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga ambao wanaiunga mkono
Urusi ameachiliwa huru katika mji wa Sloviansk nchini Ukraine.Msemaji wa kundi
hilo ameiambia BBC kwamba mwanamme huyo anayeaminika kuwa raia wa
Sweden-aliachiliwa huru kwa misingi ya kiafya.
No comments:
Post a Comment