Vijana wenye umri wa kuanzia miaka 35 na
kuendelea wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.Akizungumza
na jijini Dar es Salaam jana, mfamasia kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Goodluck Madehu, alisema vijana wa umri huo hawana utaratibu mzuri wa
kula na kufanya mazoezi.
Waziri wa
Mashauri ya Kigeni wa Marekani amelaumu Urusi kwa kuchochea mapigano Mashariki
mwa Ukraine. John Kerry alisema ujasusi wa Marekani una hakika kuwa Urusi
imetoa silaha na wapiganaji na pia inaendelea kugharamia na kusimamia wapiganaji
wa nchini Ukraine kushiriki ghasia hizo.
Rais Obama
amewasili Korea Kusini huku hofu ikizagaa kwamba Korea Kaskazini huenda
inajiandaa kufanya jaribio la nne ya zana zake za nukyla. Inatarajiwa kwamba
shughuli mpya katika kinu cha nuklya mjini Pyongyang zitatawala mazungumzo kati
ya bwana Obama na rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake. Amri iliyotolewa na Rais kupitia kwa
televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika wadhifa
wake mara moja.Hata hivyo Rais Kirr hakutoa sababu ya kumfuta kazi generali
huyo. Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba. Wiki jana
waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
No comments:
Post a Comment